Psalms 141

Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu

(Zaburi Ya Daudi)


1 aEe Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima.
Sikia sauti yangu ninapokuita.

2 bMaombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba;
kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.


3 cEe Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu,
weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

4 dUsiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya,
nisije nikashiriki katika matendo maovu
pamoja na watu watendao mabaya,
wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.


5 eMtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;
na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.
Kichwa changu hakitalikataa.

Hata hivyo, maombi yangu daima
ni kinyume cha watenda mabaya,

6 fwatawala wao watatupwa chini
kutoka kwenye majabali,
waovu watajifunza kwamba maneno yangu
yalikuwa kweli.

7 gWatasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi,
ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.”


8 hLakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi,
ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.

9 iNiepushe na mitego waliyonitegea,
kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya.

10 jWaovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,
wakati mimi ninapita salama.
Copyright information for SwhKC